Watu wanane wakiwemo raia wawili wa China wameuawa mjini Nairobi Kenya kufuatia ajali ya korongo au winchi yaani mtambo wa kunyanyua vifaa katika maeneo ya ujenzi, kuanguka. 

Mkuu wa polisi eneo la Kilimani na viunga vyake mjini Nairobi amethibitisha hayo na kuongeza kuwa watu wawili pia wamejeruhiwa wakati winchi hiyo ilipoporomoka kutoka orofa ya 14 iliyokuwa ikijengwa.

Chanzo cha winchi hiyo kuporomoka hakikubainika moja kwa moja. Ujenzi duni pamoja na ukiukaji wa taratibu za ujenzi ni miongoni mwa mambo ambayo yamesababisha ajali kadhaa kama hizo mjini Nairobi.

Mnamo Aprili mwaka 2016, watu 46 waliuawa wakati jengo la ghorofa sita lilipoporomoka kaskazini mwa Nairobi.

CREDIT:DW