Watu wawili ambao ni wanafunzi wamefariki dunia baada ya kugongwa na gari aina ya Scania wakiwa stendi maeneo ya Afrikana barabara ya Bagamoyo Wilaya ya Kinondoni.

Taarifa iliyotolewa Jumatatu Agosti 9, 2021 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro imeeleza kuwa ajali hiyo imetokea alfajiri saa 11:15 alfajiri ambapo dereva alikimbia baada ya ajali hiyo kutokea.