Wanafunzi watatu katika Shule ya Msingi Ngoile wanaoishi Kijiji cha Ngoile wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wamefariki dunia baada ya kuliwa na Simba.

Akizungumza tukio hilo leo Agosti 5,2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo amesema watoto hao wameuwa Agosti 3 mwaka huu na amewataja wanafunzi hao ni Olobiko Metui(10),Ndaskoi Sangu(9) na Sanka Saning'o( 10) ambao wote ni wanafunzi wa darasa la tatu