Wafanyakazi watano wa TRA wamefariki dunia kwa ajali ya gari mkoani Songwe alfajiri ya leo baada ya gari lao kuligonga Lori kwa nyuma.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Songwe, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo alfajiri katika barabara ya Mbeya Tunduma eneo la Hanseketwa wilaya ya Mbozi mkoani Songwe.

Taarifa za awali zinadai kuwa Watumishi hao walikuwa kazini, ambapo walikuwa wakitumia gari hiyo kufukuza gari nyingine iliyohisiwa kubeba bidhaa za magendo.