Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema idadi ya matukio ya utekelezaji wa hukumu ya kifo nchini Saudi Arabia imeongezeka tena baada ya nchi hiyo kukamilisha muda wa urais wa kundi la nchi zilizostawi na zile zinazoinukia kiuchumi duniani za G20 katika kipindi cha Desemba Mosi mwaka uliopita.

Katika ripoti yake mpya, shirika hilo limesema kati ya Januari na Julai mwaka huu watu 40 walinyongwa. Idadi hiyo ni kubwa zaidi kuliko 27 walionyongwa mwaka mzima wa 2020 wakati Saudi Arabia ilipokuwa rais wa G20. 

Naibu Mkurugenzi wa Amnesty International Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Lynn Maalouf, amesema baada ya kufuatiliwa kwa Saudi Arabia na G20 kulipopingua mamlaka za ufalme huo zilianza tena kuwaandama watu waliothubutu kutoa maoni yao kwa uhuru au kuikosoa serikali.