Shirika la watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema watoto wapatao 27 wameuawa na wengine 136 wamejeruhiwa katika majimbo matatu ya Afghanistan katika siku tatu zilizopita huku kukiwa na ghasia zinazozidi kuongezeka. 

Mwakilishi wa UNICEF Hervé Ludovic De Lys amesema shirika hilo limeshtushwa na kuongezeka kwa kasi ukiukaji wa haki za watoto nchini Afghanistan. Vifo na majeruhi vimeripotiwa katika mikoa ya Kandahar, Khost na Pakria.