==>>BI. SOPHIA SULEIMAN AENDA KUVIMBA MTAANI NA MKOKO MPYA KUTOKA TECNO
 

Hitimisho la Promosheni ya 100 Million Vimba na Camon 17 na Spark 7 ilikuwa ni Tarehe 25/08 baada ya kumshuhudia Bi. Sophia Suleiman akiibuka mshindi wa zawadi ya gari mpya, na wengine kujishindia pikipiki na majokofu.
 
“Promotion hii imechukua takribani mwezi mmoja ambapo lengo lake lilikuwa ni kutoa shukurani zetu kwa wateja wa TECNO ambao wamekuwa nasi wa takribani miaka kumi, na kwa kipindi hiki tumeamua kutoa zawadi kubwa zaidi ya gari ikiwa kama heshima na kuthamini mchango wa wateja wetu” alisema William Motta mwakilishi wa Kampuni ya TECNO.    
 
Promosheni ya 100 Million Vimba na Camon 17 na Spark 7 ilizinduliwa rasmi mnamo Tarehe 19 July ikiwa imesheheni zawadi kibao kwa wateja wote ambao walitakiwa kununua simu ya Camon 17 au Spark 7. 
 
Kila aliyenunua simu alipata zawadi za papo kwa hapo zikiwemo ear pods, Bluetooth Speakers, simu ndogo (vitochi) na zingine kibao. Wakati huo huo majina ya wateja hao yalikuwa yanaingizwa kwenye kapu la bahati kwa ajili ya kumpata mshindi wa mwisho ambaye angeibuka na gari mpya.  
 
Mshindi wetu wa gari mpya Bi. Sophia alipohojiwa na waandishi wa Habari kuhusiana na furaha yake aliyonayo alisema, “sina mengi zaidi ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwanza maana tulioshiriki ni wengi lakini mimi ndo mshindi, pili uongozi mzima wa kampuni yangu pendwa ya TECNO. 
 
"Kiukweli Mimi ni miongoni mwa watu ambao hawakuwa wakiamini katika haya mambo ya bahati nasibu na niliamini hivi vitu havipo, lakini nilishangaa sana kupokea sim una kuambiwa ni ndo mshindi. SIkutegema lakini ndo hivyo Mungu kaniona leo hii na mimi ni miongoni mwa wamiliki magari Mjini hapa hivyo ni mwendo wa Kuvimba.” 
 
Aliongeza kwa kusema; “Sijui kuendesha lakini so mda mrefu tukutane sheli kwenye foleni ya mafuta. Kwa hiyo niwashauri Watanzania wenzangu wasipuuzie michezo hii ya bahati nasibu  maana kesho yaweza kuwa wewe ndo mshindi. Asante sana.” 
 
Washindi wengine ambao kila mmoja kwa nafasi yake alikuwa na furaha  isiyoelezeka nao ni Merry Stela, Elizabeth Andrew na Castor Charse waliojishindia Jokofu na washindi wa pikipiki ni Juma Kadama na Leyla Daud.