Kampuni ya simu TECNO hivi karibuni imezindua TECNO Spark 7 moja ya toleo la TECNO lenye kuaminiwa zaidi na vijana kutokana na muundo wake lakini pia swala la bei huwa ni rafiki. Mbali na hayo kampuni Vivo nayo imezindua Vivo Y1s ikiwa inawalenga vijana zaidi.

Simu zote hizi ni bora na zinasifa nzuri lakini ni wazi kuwa huwezi kuchagua zote kwa wakati mmoja hivyo basi tumekuletea Makala ambayo itakusaidia kufanya chaguzi.
 

Kamera
TECNO Spark 7 imekuja na kamera mbili nyuma na kamera kuu ni MP16 na flash 2, ili kuifanya picha ing’ae vizuri zaidi wakati wa usiku na mbele ina MP8 na flash moja. Vivo Y1s vile vile ina kamera nyuma na mbele, kamera ya mbele ni MP5 na nyuma MP13 na flash. Kulingana na sifa hii ya kamera ni Dhahiri TECNO Spark 7 ni simu ya kununua kama uhitaji wako ni kupata picha nzuri zaidi.


Kioo

Eneo kubwa la mbele la simu ya TECNO Spark 7 limetawaliwa na wigo mpana wa kioo cha inch 6.52 HD na Vivo Y1s ina kioo cha inch 6.22 zote ni simu nzuri wigo mpana wa vioo vya simu hizi mbili utakupa uwanja mkubwa wa kuangalia movie, mpira na nyengine vingi kama kujisomea vitabu japo kwa TECNO SPARK 7 utaviona kwa ukubwa zaidi.

Battery
TECNO Spark 7 na Vivo Y1s ni simu imara zaidi kwenye swala la chaji. TECNO Spark 7 ina mAh 5000 na Vivo Y1s imekuja na mAh 4030 basi ni wadhi TECNO Spark 7 ni bora zaidi kwenye swala zima la kudumu na chaji endapo utatumia TECNO Spark 7 unauhakika wa kusiliza music na kuperuzi mtandaoni kwa zaidi ya masaa 24.

Memory
Kuepuka kero za jumbe kuwa simu imejaa basi simu zote ni sahihi kwako TECNO Spark 7 na Vivi Y1s zimekuja na memory ya GB32 na Ram GB2 kupitia simu hizi mbili unaweza kuhifadhi video, picha na application nyengine mbalimbali kama beauty camera.


Android

TECNO Spark 7 na Vivo Y1s zinatumia mfumo wa Android, TECNO Spark 7 imekuja na Android 11GO na Vivo Y1s imekuja na Android 10. Faida ya Android kubwa au naweza sema Android mpya ambayo ni Android 11 kwa mtumiaji ni hizi Android 11 ina application nyingi zaidi, inaruhusu application mpya lakini ufanisi wake ni wajuu zaidi ukilinganisha na Android za awali.

Basi hadi hapo utakuwa umeshafahamu ni simu gani inakufaa kulingana na matumizi yako.