Mbunge wa Ushetu na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Elias John Kwandikwa amefariki Dunia Jijini Dar Es salaam leo Jumatatu Agosti 2, 2021 alipokuwa akipatiwa matibabu
Katibu wa Mbunge huyo ndugu Julius Lugobi amethibitisha kutokea kwa msiba huo.
Pia Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Donald Magesa ameeleza kupokea kwa masikitiko taarifa za msiba huo.