Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya shilingi trilioni 2.7 kutoka Benki ya Dunia (WB).

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bi. Mara Warwick ndio Wamesaini mikataba hiyo kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa (IDA).

Kupitia mkopo huo, miradi itakayotekelezwa ni katika sekta ya Elimu, Barabara, Tehama na Nishati ya umeme, Tanzania Bara na Zanzibar.

Barabara za vijijini zitanufaika kwa mkopo wa Bilioni 693.2, mazingira ya elimu ya juu wa bilioni 982.1 bilioni na digitali bilioni 346.6.

Aidha,huduma za umeme Zanzibar zitanufaika kwa mkopo wa Bilioni 328.1 bilioni ukiwemo mkopo wa Bilioni 346.6 kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi visiwani humo.