Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inapenda kufahamisha umma na wadau wa Elimu ya Juu nchini kuwa awamu ya kwanza ya udahili kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa mwaka wa masomo 2021/2022 imekamilika

Waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja wanahimizwa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia kesho tarehe 24 Agosti hadi 06 Septemba, 2021 kwa namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili. 

Wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo, wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri ili kuweza kujithibitisha katika chuo husika.


Uthibitisho wa udahili ufanyike kupitia akaunti ambayo muombaji alitumia wakati wa kuomba udahili. Orodha ya majina ya waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja imewekwa kwenye tovuti ya TCU

==>Bofya hapa kupata Orodha ya majina ya waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja