Rais wa Marekani Joe Biden katika hotuba yake kwa taifa, amesema kuwa zoezi la kuondoa raia wakigeni kutoka Afghanistan itaendelea licha ya shambulio lililogharimu maisha ya watu kadhaa, hususan wanajeshi 13 wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Kabul, nchini Afghanistan.

"Amerika haitatishwa," amesema rais wa Marekani. “Hatutazuiliwa na magaidi. Hatutawaacha wazuie operesheni yetu. Tutaendelea na zoezi hilo", amsema rais wa Marekani. 

Joe Biden amebaini pia kwamba jeshi la Marekani litaondoka nchini afghanistan gosti 31 kama ilivyopangwa.
 

Joe Biden aapa "kuwasaka" washambuliaji wa Kabul
"Tutawatafuta popote walipo na tutawaangamiza," aamesema akiwaambia wahusika wa shambulio hilo, na kuongeza kuwa Marekani itajibu "kwa nguvu zote na usahihi". Askari hawa "ni mashujaa ambao walikuwa wakifanya kazi ya hatari na ya kujitolea kuokoa maisha ya watu wengine," amesema.

"Nimeagiza makamanda wangu kuandaa mipango ya kuteketeza mali ya IS-K, viongozi na vituo ya kundi hilo," Joe Biden amesema, akimaanisha tawi la IS nchini Afghanistan, kundi la Islamic State huko Khorasan.

 Kundi la Islamic State limedai kuhusika na shambulio baya lililotokea jana Alhamisi wiki hii. IS inadai kwamba mmoja wa wapiganaji wake aliweza kukaribia kwenye "mita tano za jeshi la Marekani" kabla ya kulipua mkanda wake uliokuwa umejaa vilipuzi.

Wanajeshi kumi na tatu wa Marekani waliuawa na wengine 18 walijeruhiwa, kulingana na ripoti ya hivi karibuni kutoka Pentagon, makao makuu ya jeshi la Marekani.

-RFI