Mkuu wa polisi wa Afghanistan amesema kumetokea shambulio la roketi katika kitongoji kimoja kilichoko Kaskazini Magharibi mwa Uwanja wa ndege wa Kabul katikati mwa operesheni za kuwaondoa watu na kuuwa mtoto mmoja. 

Mkuu huyo wa polisi wa Kabul anayejulikana kwa jina moja la Rashid, amesema shambulio hilo limetokea mchana wa jana jumapili na hadi sasa hakuna kundi lililodai kuhusika. 

Awali mpiganaji mmoja wa Taliban alimuua kwa kumpiga risasi muimbaji wa nchini humo katika mkoa wa milimani katika mazingara ambayo bado hayajawekwa wazi. 

Mauaji hayo yamerudisha wasiwasi miongoni mwa wanaharakati kwamba wanamgambo wa Taliban watarejea katika utawala wao dhalimu baada ya kuiangusha serikali. 

Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid amelieleza shirika la habari la AP kuwa watachunguza tukio hilo, lakini hawakuwa na maelezo mengine juu ya mauaji.