Ili mapenzi yanoge basi ewe mwanamke  unatakiwa kuhakikisha ya kwamba unafanya mabo yafutayo kwa mumeo;

1.Muamini mmeo au mchumba wako. 
iongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakivunja mahusiano ya watu wengi katika karne hii ni pamoja na kukoseana kwa neno uaminifu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Jambo hili limekuwa likiwakuta kwa asilimia kubwa wanawake, yaani utakuta mtu anamuliza mume wake upo wake, hata mumewe ataje sehemu sahihi aliyopo bado mwanamke huyo hata amini vile vile.

Hivyo watalamu wa masuala ya mahusiano na mapenzi kwa ujumla nikiwemo na mimi natumia wasaa huu kukushauri ya kwamba unatakiwa kujenga imani na mumeo ili muweze kujenga mahusiano yenu thabiti kwani kumuanini mpenzi wako ndiyo siraha makini itakayowasiadia muweze kudumu zaidi katika mahusiano yenu.

2.Usimkatishe tamaa katika maono yake. 
Kila wakati unatakiwa kuelewa mwanaume hupenda mwanamke mwenye akili, mwenye uwezo wa kushauri mambo ya kimafanikio kila wakati, hakuna mwanaume ambaye hapendi kukatishwa ndoto zake kwa sababu ya mawazo ya mwanamke.

Hivyo kila wakati yakupasa kuelewa ya kwamba kama unataka kufanikiwa hatimaye kufikia mbali katika mahusiano yenu basi unatakiwa kuelewa kwamba unatakiwa kupambana kila wakati kwa namna moja ama nyingine katika suala la kupambana ili kuhakikisha unatimiza ndoto na maono za mumeo.

4.Usilazimishe mwanaume kuwajibika juu ya mambo yako.
Kama vile kwenda saluni, umeme, vocha na mambo mengine hasa kama bado mko katika mchakato wa uchumba, kama atafanya hivyo mwache afanye mwenyewe msimlazimishe eti kwa sababu shosti wako huwa anafanyiwa hivyo na wewe unataka, ladies huo ni utoto.

Kumbuka ya kwamba wanaume hawafanani tabia, wengine hawapendi kushulutishwa, hii ni kwa sababu wapo wanawake wengine wao hudhani kila kitu ni lazima afanyiwe na mwanaume, no hata wewe unao uwezo wa kujihudumia baadhi ya vitu. Pale mwanaume anapokuwa ameeamua kukusaidia kufanya jambo fulani basi huna budi kulipokea kwa mikono miwili.

Ukiyazingatia hayo mwanamue huyo atakupenda milele hadi utaona kama dunia hii umeumbiwa wewe na huyo mwenza wako pekee.