Mara nyingi unapokuwa katika mahusiano ya kimapenzi basi mwanaume ambaye hana malengo na wewe katika mahusiano yenu basi utmajua kwa kuangalia mambo yafuatayo;

1.Anakwepa mazungumzo ya ndoa.
Haonyeshi kufurahi unapoanzisha mazungumzo kuhusu suala la kufunga ndoa na wala hapendi kuzungumzia hilo. Wakati mwingine hata kukutambulisha kwa ndugu zake au rafiki inakuwa shida.

2.Anagharamia anasa kuliko mambo muhimu.
Anakuwa ni mtu wa kukununulia mapambo ya gharama na vitu vyote vya anasa, lakini hana mawazo ya kuzungumzia maisha yenu ya baadaye wala kukununulia vitu ambavyo vitakuwa na manufaa katika maisha ya mbeleni. Haangalii masuala ya elimu wala kukutafutia mtaji au kazi.

3.Hajali machozi yako.
Unaweza kugundua ni jinsi gani hana mpango mzuri na maisha yako, kwani hata anapokuudhi anakuwa hajali wala haumizwi na machozi yako, ni busara kuwa makini kwa sababu huyo atakuwa ni mtu wa kukupa maumivu wakati wote.

4.Hajitokezi hadharani
Mwanaume ambaye malengo yake ni kukuchezea huwa hataki mapenzi yenu yajulikane hadharani atakuwa mtu wa kutaka mambo yaende kwa siri. Hajitambulishi kwa rafiki wala kwa ndugu zako. Hatoi nafasi ya wewe kumtembelea nyumbani kwake wala kuwajua wale wa karibu yake na familia yake.

5.Hana mpango na watu wako
Mwanamume anayekupenda atajishughulisha na mambo yanayohusiana na watu wako wa karibu, hususan ndugu, jamaa na marafiki zako.  Utabaini kuwa mwanamume huyu haulizi swali lolote kuhusiana na familia yako au marafiki zako, basi tambua kuwa hana mpango wowote wa maana na wewe. Kumbuka mwanamume akikupenda hujaribu kuwafahamu na kuwapenda watu wako, maana amependa boga na sheria ni kwamba lazima upende na ua lake.

6.Hakumbuki lolote la maana
Ni wazi kuwa hujakaa sana na mwanamume huyu, lakini angalau kuna mambo muhimu umefanya naye ambayo anapaswa kuyakumbuka. Kama hawezi kukumbuka tarehe muhimu za uhusiano wenu,  basi yamkini mwanamume huyu hana mpango wowote wa dhati wa kuendelea kuwa nawe.