Mfanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite na mmiliki wa mgodi wa Manga Gems, Mathias Manga amefariki dunia akitibiwa nchini Afrika Kusini.
 

Bw.Mathias aliwahi kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM(NEC) na diwani wa kata ya Mrangarini wilayani Arumeru

Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Manyara, Sadick Mnenei amesema wamepokea taarifa za kifo cha Manga aliyekuwa anayemiliki mgodi wa Tanzanite wa Manga Gems uliopo kitalu D, jana mchana.

"Ni kweli tumepata taarifa za kifo kutoka Kwa watu waliokuwa karibu naye na alikuwa anaumwa hata kupelekwa huko kwa matibabu," amesema.

Manga pia alikuwa anaendesha Hoteli za Gold Crest zilizopo jijini Arusha na Mwanza na alikuwa anamikiki majumba kadhaa ya kifahari jijini Arusha..