Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 34, amepangwa kufanyiwa vipimo vya matibabu hii leo Jumatatu kabla ya kukamilisha uhamisho wa bure kwenda Paris St-Germain. 

Messi atazinduliwa kama mchezaji wa PSG kwenye hafla maalum katika Mnara wa Eiffel katika siku chache zijazo. 

Barcelona wanajaribu kuzuia jaribio lolote la PSG kumsaini Messi kwa kufungua malalamiko kwa Tume ya Ulaya ikisema kilabu hiyo ya Ufaransa itakiuka sheria za matumizi ya fedha ikiwa watafanikiwa kumsajili Muargentina huyo. 

Tottenham ni miongoni mwa vilabu ambavyo vimejaribu kumsajili Messi baada ya Barca kusema hatosalia Nou Camp.