Club ya PSG ya Ufaransa imemtambulisha rasmi Lionel Messi (34) kama Mchezaji wake mpya na kusaini mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja zaidi.

Messi ametambulishwa na kupewa jezi namba 30 ambapo hajataka kumvua jezi namba 10 Neymar kwa heshima ya swahiba wake huyo na kuamua kutumia jezi namba 30 aliyoanza kuitumia kwa mara ya kwanza Barcelona.

Mara nyingi Staa mkubwa anapojiunga na timu mpya hupewa namba ya jezi yake pendwa hata kama ina Mtu mwingine na imewahi kutokea kwa wengi kama Samatta na Ozil ndani ya Fenerbahce na hata Juventus alipowasili Ronaldo jezi namba 7 akaichukua kutoka kwa Juan Cuadrado.