Mchambuzi Nguli Wa Soka Nchini, Mwalimu Kashasha Afariki Dunia
Mchambuzi maarufu wa soka, Mwalimu Theogenes Alex Kashasha amefariki dunia leo Agosti 19, 2021 akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Kairuki mkoani Dar es Salaam.
Kashasha alikuwa mtumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) hadi umauti ulipomfika.