Upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu umepanga kutumia mashahidi 24 na vielelezo  19.

Hayo yameelezwa leo, Agosti 23, 2021 na upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga akisaidiana na Ester Martin, wakati wakiwasomea maelezo ya mashaidi na vielelezo washtakiwa hao, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba.