WATU wengi nchini wamekosa ajira  kwa sababu ya makosa wanayoyafanya wakati wa kuandika na kutuma maombi ya kazi.


Kumbuka,  makampuni  karibia yote yanayotangaza nafasi za kazi hupokea wastani wa maombi 500-1000 ya kazi kwa tangazo moja la kazi. 

Sasa, dunia imebadilika. Zaman tulikuwa tunatumba maombi ya kazi kwa njia ya posta. Saiv makampuni mengi yanakutaka utume maombi yako ya kazi kwa njia ya Email/Barua Pepe.

Ni vipi basi utatuma maombi yako ya kazi kwa Email? Mambo gan ya msingi unatakiwa kuzingatia? Je, utaweka tu ma documents uliyoagizwa na kuyatuma pas kufanya lolote?

Kwa hayo yote na mengine, ungana nami hapo chini

==>>Mambo ya kuzingatia wakati wa kutuma maombi kwa njia ya Email/Baruapepe.

1.Tumia email yenye majina yako rasmi. Mfano kama wewe ni Richard John, jitahidi email yako  iwe hivi; richardjohn@gmail.com au rjohn@gmail.com.
Unaweza hata kuongeza namba kama majina yako mawili hayapatikani. Kumbuka hii itaongeza kuaminiwa na mwajiriwa mtarajiwa kuliko kutumia email kama; misslove@gmail.com, cutebabylina@gmail.com, kidumejogoo@gmail.com...NK  

 
2. Tumia  email zinazokubalika kimataifa. Mfano, sishauri watu kutumia email za microsoft au  yahoo . Haina usalama sana, na mifumo mingi huziblock. Tumia Gmail
   

3.Elezea vizuri kwenye kichwa cha habari yaani subject ya email unaomba nafasi gani ya kazi. Soma tangazo la kazi ulielewe vizuri, then andika kwa usahihi kazi unayoimba. Makampuni mengi hustoa  kabisa kichwa cha kazi unayotaka kuomba, kwa hiyo unatakiwa kukopi na kupaste. Usipofanya hivyo maombi yako yanaweza kuachwa .
 

4.Kwenye  'body' ya email  au mesage eleza wewe ni nani? Umezipataje hizo taarifa za nafasi za kazi?Unafikiri wewe utapeleka kitu gani nzuri ambayo wengine walioomba hiyo nafasi hawana ila wewe unayo/unazo.

Eleza utayari wako wa usaili na kuanza kazi. Pia eleze kwa ufupi:Kiwango chako cha elimu (elezea tu ya hivi karibuni na inayoendana na kazi uliyoomba), Uzoefu wako wa kazi (elezea tu ya hivi karibuni na inayoendana na kazi uliyoomba).

Acha mawasiliano yako ya haraka kama simu ya kiganjani na barua pepe (usiache mawasiliano ya kupitia kwa watu wengine kama shangazi mjomba, mama, baba na marafiki au jirani).
    

5.Weka viambatanisho tu ambavyo ulielekezwa utume, vile ambavyo hukuambiwa usitume maana vinaweza kukukosesha kazi. Waajiri wengi siku hizi wanapunguza mzigo wa maombi ya kazi ikiwa ni pamoja na package nzima ya maombi lakini pia na wingi wa waombaji. Ni rahisi sana kuchujwa kwenye chujio la mwanzo kama wewe umekiuka masharti ya wazi tu.
    

6. Kwenye viambatanisho hakikisha vyote vina majina yanayoendana na kilichomo ndani. Mfano kama umeambatanisha Barua ya Maombi ya Kazi ya Afisa Masoko, weka jina la faili liwe na hayo maneno. Kama umeambatanisha CV kwenye filename ya CV weka CV ya jina lako.

7.Pia, hakikisha viambatanisho vyako vinakuwa katika mfumo wa PDF. Usime kwa Microsoft Word .Hii itapunguza usumbufu maana huwezi jua mwajiri anatumia toleo gani na Word Document.

Baada ya maelezo hayo kina, hapo chini nimekuwekea mifano zaidi ya 20 ya namna ya kutuma maombi ya kazi kwa Email pamoja na mifano ya barua za maombi kwa Email.

==>>Bofya HAPA Kutazama Mifano mbalimbali (Kwa kiingereza) ya namna ya kutuma maombi kwa Email.


==>>Je,unatafuta kazi? <<Bofya hapa>>. Zipo nafasi za kazi serikalini, Makampuni Binafsi,NGOs mbalimbali