Na Lucas Raphael,Tabora 

JESHI LA polisi mkoani Tabora linawashikilia watu watatu wakiwemo mume na watoto wake wawili kwa kula njama za kuumua mama yao na mume kuumua mkewe       aliyetambulika kwa ajina la Maria Kishiwa baada ya mwanamke huyo kuungua maradhi kwa muda mrefu waliona kero hivyo wakalazimaka kummalizaia mbali mama huyo .

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoani Tabora Safia Jongo alisema kwamba tukio hilo lilitokea agasti 3 mwaka huu  Asubuhi katika kijiji cha Isalalo kata ya Utwigu wilaya ya Nzega mkoani hapa .

Alisema kwamba chanzo ni kuugua maradhi kwa muda mrefu na mbinu iliyotumika ni kumfanga kamba shingoni na kumninginiza ili aonekane kuwa amejinyonga.

Alisema kwamba Maria alikuwa amefariki akiwa amefungwa kamba shingoni huku akininginia na kamba ikiwa imefungwa kwa kukazwa kwenye nguzo ya jiko kitu ambacho marehemu hakuwa na nguvu kiasi hicho baada ya kuugua kwa muda mrefu

Hata hivyo kamanda huyo wa polisi  alisema kwamba baada ya kumninginiza marehemu waliacha kinu na kigoda bila kuanguka chini ili kuonyesha kuwa ndipo alipopanda na kujinyoga .

 “Wakati ni vigumu kwa mtu mgonjwa kupanda hadi kuwe na masada wa watu wengine jambo ambalo lilileta mashaka “ alisema kamanda Safia .

Alisema kwamba marehemu Maria alikuwa analala na mjukuu wake ambaye alifichwa ili asibaini mbinu hiyo ya mauaji jambo hilo ndilo lilipelekea polisi kuanza kuchuguzi ambapo mjukuu huyo alisema kila kitu kilichofanyika kumuua bibi yake.

Alisema kwamba majina ya watu hao watatu yamehifadhi kwa ajili ya uchuguzi mzima wa tukio hilo la kinyama

Hili nituo la pili kutokea katika wilaya ya nzega kwa muda wa usiozidi wiki Tatu baada ya watoto wawili wakiwa wanachunga mifugo kuuawa na kufukiwa kwenye shimo ili kupoteza ushaidi.