Zaidi ya nyumba 1,000 zimeharibiwa na watu 5,000 wameokolewa baada ya kutokea mafuriko ya maji, ambayo yamesababishwa na mvua kubwa huko Korea Kaskazini.

Naibu mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini humo, Ri Yong Nam amesema mvua kubwa zinatarajiwa kuendelea katika mikoa mbalimbali nchini humo hadi Agosti 10 na hasa katika maeneo ya pwani ya mashariki.

Televisheni ya umma ya taifa hilo imetangaza pia maeneo ya mashamba yamefunikwa na maji. Taarifa hiyo inatolewa baada ya taifa hilo Juni kukiri kukabiliana na tatizo la chakula.

Na mwezi uliopita Shirika la Chakula na Kilimo FAO lilionesha kwamba Korea Kaskazini inakabiliwa na upungufu wa takribani tani 860,000 ya chakula kwa mwaka huu na kulionya taifa hilo kupitia kipindi kigumu.