Ofisi za Kituo kikubwa cha kupokea na kusambaza umeme Msamvu - Morogoro limewaka moto na kusababisha Mkoa wa Morogoro kukosa umeme.

Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika, lakini taarifa ya TANESCO imeeleza kuwa wataalamu  na mafundi wanaendelea na kazi ya kuhakikisha huduma ya umeme inarejea kwa haraka.