Kwa takribani wiki kadhaa sasa zimepita tangu Promosheni ya Kuli Kuliko kutoka Infinix imeanza. Na hitimisho lake ilikuwa siku ya Jumamosi Tarehe 28.8.2021 baada ya kushuhudia wateja wakijinyakulia zawadi zao kutoka Infinix. Zawadi zilikuwa katika mgawanyiko wa makundi mawili ambayo ni Zawadi Kubwa zilizotoka siku ya hitimisho na zawadi za papo kwa hapo ambazo hizi mteja alikuwa napewa pale tu anapo nunua simu.
Zawadi kubwa kabisa ilikuwa ni PS5 mpya, TV za 55”, Microwave, Laptop nk. Washindi wa zawadi hizi ni wale walionunua simu za Infinix na majina yao yaliingia kwenye droo iliyo chezeshwa na mwisho wa siku kupatikana washindi. Akiongea na vyombo vya habari Meneja wa Promosheni Ndg. Joseph Vigambo alisema “Tumepata maoni mengi kutoka kwa wateja wetu kwamba promosheni imeenda vizuri lakini muda ulikuwa ni mfupi sana wanatamani kwa inayofuata iongezwe muda kidogo.” Pia aliongeza kwa kusema “hamasa na ushiriki ulikuwa mkubwa sana na watu walifurahia sana hasa mchezo wa kupiga dana dana. Wito wangu kwa wateja wetu wote ni ” 
 

Bwana Hery Barnabas ambaye ndiye alieibuka kidedea na kujinyakulia zawadi ya PS 5 (ambayo ndiyo ilikuwa zawadi kubwa) alikuwa na haya ya kusema ”binafsi nimefurahi sana kwa hii zawadi maana ni kitu ambacho sikutarajia. Kumbe ni kweli uwezekano wa mtu yoyote kujishindia zawadi katika hizi bahati nasibu upo maana mimi kutoka kampuni ya Infinix hakuna anaenifahamu lakini nimekuwa mshindi.” Sambamba na hilo Bwana Hery alikuwa na shukrani zake kwa uongozi mzima wa Kampuni ya Infinix. Aliongeza kwa kusema “nipende kutoa shukrani zangu za dhati kwa kampuni kwa kuniwezehsa kupata zawadi hii ambayo ni kitu kikubwa sana kwangu. Asante”  

 

Miongoni mwa washindi wengine ni Bwana Salim na Rajab ambao ndo walikuwa washindi wa TV mpya yenye yenye ukubwa wa 55”
 
Zawadi nyingine zilizoenda kwa washindi ilikuwa ni pamoja na Laptop, microwaves, majagi ya kuchemshia maji, nk.
 
“Wito wangu kwa wateja wetu ni kutokupuuzia mashindano kama haya maana yawezekana kesho ukawa wewe ndiyo mshindi hivyo inapotoke ukapata nafasi ya kushiriki usipuuzie. Karibuni sana na kututane msimu ujao.” Alimaliza kwa kusema hivyo Promosheni Meneja wa Infinix.