Jeshi nchini Indonesia limeondoa kipimo cha bikra kwa wanawake wanaojiunga na jeshi mkuu wa utumishi jeshini ametangaza jana. Mkuu huyo wa utumishi Andika Perkasa amewaambia waandishi wa habari kwamba iwapo mwanamke atakuwa na bikra ama la kipimo hicho hakitaendelea kufanyika.
Huko nyuma jeshi nchini humo lilitumia kipimo hicho kufanya maamuzi kuhusu uadilifu wa waajiriwa hatua iliyokuwa ikipingwa kwa muda mrefu na makundi ya haki za binaadamu wakisema inashusha utu na ni ya kufadhaisha.
Shirika la Human Rights Watch lilifanya uchunguzi kuhusiana na utamaduni huo iliouita wa kimfumo wa kinyanyasaji na wa ukatili wakati shirika la afya ulimwenguni, WHO likisema vipimo hivyo havina uthibitisho wowote wa kisayansi.