TECNO Spark 7 kutoka Kampuni ya simu TECNO ni kati ya simu bora iliyozingatia zaidi mahitaji ya mtumiaji. TECNO Spark 7 pamoja ya kuwa na sifa zote muhimu kama memory ya GB 32Rom + 2Ram, battery mAh5000, kamera ya nyuma 16MP, 8MP Selfie, Android 11GO na inch 6.52 Dot Notch lakini ni simu inayopatikana kwa bei rafiki. Bila ya kupoteza muda tufahamu umuhimu wa kila sifa kama nilivyoorodhesha hapo juu.
 

Kamera
TECNO Spark 7 imekuja na kamera mbili nyuma na kamera kuu ni MP16 na flash 2 kwa mbele TECNO Spark 7 ina MP8. Kamera za simu hii zinauwezo wakuchukua picha wakati wowote lakini pia tecknolojia ya AI inafanya Camera ya TECNO Spark 7 kupiga picha zenye rangi halisi.

Kioo
Eneo kubwa la mbele la simu ya TECNO Spark 7 limetawaliwa na wigo mpana wa kioo cha inch 6.52 katika swala zima la kuangalia movie, mpira basi si tatizo tena endapo unatumia simu hii. TECNO Spark 7 pia ni simu sahihi kwa wanafunzi kwani kupitia simu hii unaweza jisomea vitabu na Makala mbalimbali kwa ukubwa zaidi.




Battery
TECNO Spark 7 ni simu imara zaidi kwenye swala la chaji haijalishi matumizi yako ni makubwa kiasi gani lakini kupitia battery ya mAh5000 unauhakika wa kufanya yote kwa siku nzima pasipo simu kuzima chaji. Kesha mtandaoni ukiperuzi, furahia music wakati wote na cheza games na TECNO Spark 7.

Memory
Kuepuka kero za jumbe kuwa simu imejaa basi tumia TECNO Spark 7 kupitia GB32 kwa ram ya GB2 unauwezo wa kuhifadhi video, picha na application nyengine mbalimbali kama beauty camera n.k. tumia TECNO Spark 7 uepukane na gharama zaidi ya memory card ya ziada.



Android
TECNO Spark 7 inatumia latest Android ambayo ni Android 11, Android 11 GO faida zake kuu kwa mtumiaji; mtumiaji anapata application nyingi zaidi na hata ambazo ni mpya mtumiaji wa Spark 7 bado anayonafasi ya kuzidownload lakini pia ufanisi wa simu ya Android ni tofauti na Android za awali.

Tembelea https://www.tecno-mobile.com/tz/home/#/