Staa wa muziki Bongo na Africa Diamond Platnumz ametoa ya moyoni kuhusu kitendo cha aliyekuwa Afisa habari wa Klabu ya Simba kuacha kufanya kazi hiyo katika klabu hiyo yenye maskani mitaa ya Msimbazi Kariakoo.


Kupitia Instagram yake Diamond ameeleza haya; “Ukiachana na  Upenzi wangu wa team ya Simba ambao kiukweli umetokana na ushawishi wako… lakini kama Mtanzania ninaependa maendeleo ya tasnia ya michezo, nimeumia kutokuwepo kwako tena simba.

“Licha ya kuiongezea Hamasa, ushawishi timu yetu ya Simba, lakini kupitia mbwembwe zako za usemaji, utani kwa Yanga na timu mbalimbali ulifanya tasnia ya michezo kuchangamka zaidi na hata ambao tulikuwa si wafatilia kandanda kuanza kufatilia, kuhudhuria na kwa namna moja au nyingine tasnia ya mpira wa miguu kuongezeka pato zaidi.

“Inshallah mwenyezi Mungu ajalie kheri yake siku moja haya yote yaishe na urejee tena kuwa msemaji wa SIMBA…kwasababu kiukweil kwa shabiki wa kweli wa Simba kuondoka kwako lazima  kumuumize, maana thamani ya mchango wako Simba unafahamika…..Inshaallah Mwenyezi Mungu azidi kukufungulia kheri, akulinde na akuepushe na kila baya.”