Kampuni za kutengeza chanjo ya COVID-19 za Pfizer na Mordena zimepandisha bei ya chanjo katika mikataba yake mipya ya mauzo na Umoja wa Ulaya. 

Ripoti iliyochapishwa na gazeti la Financial Times iliyotolewa siku ya Jumapili imenukuu sehemu ya makubaliano hayo, ikisema bei mpya ya chanjo ya Pfizer imepanda hadi euro 19.50 kutoka euro 15.50 za awali. 

Gazeti hilo limemnukuu afisa mwenye uelewa na suala hilo, na kusema dozi ya chanjo ya Mordena iliyokuwa ikiuzwa dola 25.50, itauzwa dola 28.50 kwenye makubaliano hayo mapya, na hii ni kutokana na ongezeko la mahitaji. 

Juhudi za shirika la habari la Reuters za kupata tamko kutoka kwa kampuni ya Pfizer na Moderna hazikufanikiwa.