Wakati chanjo ya corona ikiendelea kutolewa katika Mataifa mbalimbali Duniani, chanjo ya Virusi vya UKIMWI (VVU) iliyokuwa inafanyiwa utafiti muda mrefu na Kampuni ya Moderna ya Marekani inatarajiwa kuanza kufanyiwa majaribio kwa Binadamu leo Jumatano.

Kampuni hiyo imetengeneza chanjo za aina mbili za UKIMWI ambazo zimefuzu hatua za awali za kimajaribio na hivyo kuanza kutumika kwa binadamu katika awamu ya tatu, chanjo hizo ni mRNA-1644 na mRNA-1644v2-Core ambazo zimeshachunguzwa na kufanyiwa majaribio ya awali na kuonekana salama kabla ya kujaribiwa kwa Binadamu kwa mara ya kwanza.

Chanjo hiyo itaanza kutolewa kwa Watu 56 wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 56 na majaribio yanatarajiwa kukamilika Mwaka 2023.