Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Amosi Makala ameagiza wamiliki na wasimamizi wa vyombo vya usafiri kuhakikisha wanatekeleza miongozo iliyotolewa na Wizara ya Afya juu ya kujilinda na ugonjwa wa Corona baada ya tathmini kuonyesha asilimia kubwa ya miongozo haitekelezwi.

Mkuu wa mkoa ametoa agizo hilo jana baada ya kikao na viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani humo kufuatia kusua sua kwa utekelezaji wa maagizo hayo ikiwa ni pamoja na watu kutovaa barakoa katika vyombo vya usafiri.

Kwa upande wa wanafunzi mheshimiwa makala amesema ili kuepusha changamoto kwao ameagiza waruhusuwe kuingia watano ila lazima waliovaa barakoa.

Kuhusu suala la Chanjo RC Makalla amefurahi kuona Wananchi wamekuwa na mapokeo makubwa ya kupokea chanjo ambapo kwa Mujibu wa Mganga mkuu wa Mkoa huo  tayari Wananchi 10,000 wamefanya booking na wanahofia Chanjo zitawahi kumalizika.


BONYEZA HAPA KUJUA VITUO VITAKAVYOTOA CHANJO YA CORONA TANZANIA