Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwenye Serikali ya awamu ya nne, John Mwakipesile, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Agosti 17, 2021.


Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Ismail Mlawa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya, Jacob Mwakasole, wamethibitisha kupokea taarifa za msiba huo kwa masikitiko makubwa na kusema kuwa ni pigo kubwa kwao.

Marehemu Mwakipesile alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya wakati wa uongozi wa wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.