Hali ya hewa imeendelea kuwa mbaya nchini Ujerumani ambapo watu zaidi ya 30 wamekufa na wengine kadhaa hawajulikani walipo. Miongoni mwa waliokufa walikuwa wazima moto wawili. 

Wanajeshi wamepelekwa kwenye sehemu zilizoathirika zaidi na pana hofu huenda idadi ya vifo ikaongezeka wakati juhudi za kuwahamisha watu zinaendelea. 

Watu waliokufa walishindwa kuondoka mapema kwenye sehemu zilizokumbwa na mafuriko za magharibi mwa Ujerumani. Mafuriko hayo yamesababishwa na mvua kubwa iliyonyesha jana kutwa. Baadhi ya nyumba zilizolewa na mafuriko na watu kati ya 50 na 70 hawajulikani waliko. 

Idara kuu ya utabiri wa hali ya hewa imetahadhrisha juu ya mvua kubwa kuendelea kunyesha leo itakayoandamana na dhoruba na kwamba mvua hizo zitaendelea hadi kesho jioni. 

Kansela Angeka Merkel aliyeko safarini amesema amewasiliana na wizara za mambo ya ndani na fedha kutoa misaada pale itakapohitajika.