Watu wenye silaha wamewateka nyara wanafunzi zaidi 140 kutoka shule ya kulala huko KaskaziniMagharibi mwa Nigeria. Ripoti hiyo ni kwa mujibu wa afisa wa shule aliyefahamisha, ikiwa ni wimbi la karibuni kabisa la utekaji nyara unaowalenga watoto wa shule na wanafunzi. 

Magenge makubwa ya wahalifu wenye silaha mara nyingi hushambulia vijiji na kufanya uporaji,kuiba mifugo pamoja na kuwateka nyara watu kwa lengo la kudai kulipwa kigombozi huko Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo ya Nigeria na eneo la kati mwa nchi hiyo. 

Hata hivyo katika kipindi cha mwanzoni mwa mwaka huu matukio ya utekaji nyara wanafunzi kwenye shule na vyuo yameongezeka. Washambuliajo wamevunja ua na kuingia katika shule ya sekondari ya kulala ya Bethel Baptist katika jimbo la Kaduna leo Jumatatu na kuondoka na wanafunzi 140. 

Msemaji wa polisi katika jimbo hilo Mohammed Jalinge a,ethibitisha tukio hilo lakini hakuweza kutoa maelezo zaidi kuhusu idadi ya wanafunzi waliochukuliwa mateka.