Shirika la udhiti wa dawa la Ulaya EMA, limependekeza kuidhinishwa kwa chanjo ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona ya Moderna kutumika kwa watoto walio na umri wa miaka 12 hadi 17. 

Hii ndiyo mara ya kwanzha chanjo hiyo kuidhinishwa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. 

Katika uamuzi uliotolewa leo shirika hilo la kudhibiti dawa barani Ulaya limesema uchunguzi uliofanywa kwa zaidi ya watoto 3,700 kati ya umri huo unaonyesha kwamba chanjo ya Moderna inatoa kinga dhidi ya virusi hivyo. 

Chanjo hiyo tayari imeidhinishwa kutumika kwa watu wote wazima kote barani Ulaya. 

Hadi sasa chanzo inayotengenezwa na kampuni ya Pfizer na mshirika wake wa Ujerumani BioNTech ndiyo chanjo ya pekee iliyokuwa imeidhinishwa kutolewa kwa watoto Marekani na Ulaya. 

Marekani bado inatafakari iwapo iidhinishe chanjo hiyo kwa watoto.