Shirika la Afya Duniani WHO linasema bara la Afrika limeathirika vibaya zaidi na janga la virusi vya corona wiki hii ila hali bado itakuwa mbaya zaidi huku wimbi la tatu la maambukizi likishika kasi barani humo. 

Dokta Matshidiso Moeti ambaye ni mkurugenzi wa WHO Afrika amesema maambukizi katika bara hilo yanaongezeka maradufu kila baada ya siku 18 ikilinganishwa na kila siku 21 wiki moja iliyopita. 

Moeti amesema ongezeko hili la maambukizi halitoisha hadi baada ya wiki kadhaa. Katika wiki iliyoisha Julai 4 pekee, Afrika iliandikisha zaidi ya maambukizi 250 elfu hiyo ikiashiria ongezeko la asilimia 20 ikilinganishwa na wiki moja kabla. 

Nchi 16 za Afrika sasa zinashuhudia maambukizi kuongezeka huku aina mpya ya kirusi cha Delta kikidaiwa kuwa kati ya nchi 10 kati ya hizo 16.

CREDIT:DW