Mtu anaposhindwa kufanya tendo la ndoa kutokana na wasiwasi kinachotokea ni kuwa mtu huyu anaacha kushiriki kikamilifu na mwenziwe. 

Mtu huyu anaacha kuweka akili yake kwenye mawazo ya kumpa ashiki na kutosikilizia vionjo vinavyoambatana na uwepo wake wa faragha wa yeye na mpenziwe. 

Badala ya kuwa na fikra za ashiki, anapeleka mawazo yake nje na kufikiria ni nini kitatokea iwapo atashindwa kulikamilisha tendo, ni vipi mwenziwe atamchukulia kuhusu urijali wake na jinsi mpenzi wake atakavyomchukulia kiujumla. 

Ataanza kupata wasiwasi kuwa kwa kuwa ana tatizo la jogoo kushindwa kuwika au kwa kukosa kufika kileleni basi mpenzi wake wa kike au wa kiume atamhesabu kuwa si mwanamme au mwanamke kamili.

Kupata ashiki kunaendana na kiwango cha utulivu wa ubongo wako. Hata kama mwenzi wako atakuvututia kwa kiwango gani, mijadala ndani ya ubongo wako kuhusu uwezo wako wa kumridhisha, itasababisha ushindwe kumudu kufanya tendo la ndoa kikamilifu.

Kwa wanaume, moja ya matokeo ya uwepo wa homoni za kuleta msongo wa mawazo (stess hormones) ni kuiminya mishipa ya damu. 

Damu itatiririka kwa kiwango kidogo sana kuelekea kwenye uume na kuufanya uume kushindwa kusimama imara. Hata uume wa mwanamme wa kawaida unaweza kushindwa kusimama na kuishia kupata tatizo hili.

Tatizo la kushindwa kufanya mapenzi kutokana na wasiwasi haliwasumbui sana wanawake ukilinganisha na wanaume, lakini linaweza kumzuia mwanamke kufikia utayari wa kufanya mapenzi. 

Wasiwasi unaweza kuzuia mwanamke asitokwe na ute wa kutosha wa kumfanya afurahie tendo la ndoa, na unaweza kuuzuia mwili wake kupenda kufanya mapenzi.

Tatizo la kushindwa kufanya mapenzi kutokana na wasiwasi ni la mzunguko usioisha kwa maana kwamba ukianza kuwa na wasiwasi kiasi cha kushindwa kufanya mapenzi, hali hiyo itakufanya uwe na wasiwasi zaidi na zaidi wa kulifanya tendo hilo.

Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha tatizo hili. Kwa kawaida, kama tatizo hili lilishawahi kujitokeza siku za nyuma, litachangia kwa kiasi kikubwa hali ya sasa hivi. 

Lakini, kwa kiwango kikubwa, tatizo la kushindwa kufanikisha tendo la ndoa kutokana na waswasi linatokana na wasiwasi wenyewe.

1.Wasiwasi ya kuwa hutafanya vizuri na kushindwa kumridhisha mpenzi wako kitandani.

2.Kuwa na wasiwasi kuhusu umbo lako la mwili, pamoja na unene wa kupindukia

3.Matatizo katika mahusiano yenu

4.Wasiwasi wa mwanamme kuwa uume wake ni mdogo

5.Wasiwasi wa mwanamme wa kumaliza mapema au kuchukua muda mrefu mno kufika kileleni

6. Wasiwasi wa mwanamke wa kushindwa kufika kileleni au kulifurahia tendo la ndoa

Mambo mengine yanayoweza kuchangia ni:
.
 Msukumo Wa Jamii
Msukumo wa jamii ni moja ya sababu kubwa za wasiwasi wa kufanya tendo la ndoa. Wanaume wanafikiri kuwa kushindwa kuwaridhisha wanawake kutawapunguzia mwonekano wao katika jamii na wanawake pia wanafikiri wanaume watawajadili kulingana na maungo yao na uwezo wao wa kufanya mapenzi. Hali hii inachochewa na jinsi watu wa karne hii wanavyoonyesha mambo ya siri hadharani na kulifanya tatizo hili kuwa kubwa zaidi kila siku.

. Kukosa Uzoefu
Kukosa uzoefu katika mapenzi kunaweza kusababisha matatizo madogomadogo katika kufanya tendo na baadaye kumsababishia mtu kupatwa na tatizo la kuwa na wasiwasi wa kufanya tendo la ndoa. Kuwahi kufika kileleni, kwa mfano, ni tatizo la kawaida kwa wale wasio na uzoefu wa kufanya mapenzi na likitokea husababisha aibu, na taratibu huanza kumjengea wasiwasi mhusika na baadaye kuishia na matatizo makubwa katika ufanyaji mapenzi.

Kukutana Kimapenzi Kulikoleta Mtafaruku
Tendo la ndoa mtu hulifanya akiwa na matarajio. Kwa hiyo mtu ambaye aliwahi kugombana, kuwa na mabishano makubwa, au kuadhiriwa na mpenzi wake kwa sababu yo yote wakiwa chumbani anakuwa kwenye hatari kubwa ya kuwa na wasiwasi watakapokutana na mtu mwingine kimapenzi. Kwa kawaida watu wapo makini sana kuhusu uwezo wao wa kufanya mapenzi, miili yao n.k. na kitu cho chote kitakachowavuruga kuhusu haya, kitawaletea wasiwasi.