Kiongozi wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni Papa Francis ametangaza kuwa ataitembelea Slovakia mwezi Septemba baada ya kufanya safari fupi nchini Hungary ya kusherehekea misa katika mji mkuu Budapest. 

Baba Mtakatifu amewaambia waumini katika Kanisa la Mtakatifu Petero mjini Rome leo kuwa atafanya ziara nchini Slovakia tarehe 12 hadi 15 Septemba. 

Ziara ya Papa Francis nchini Slovakia itajumuisha miji ya Bratislava, Presov, Kosice na Sastin. Rais wa Slovakia Zuzana Caputova alimualika Papa Francis wakati alipokutana na kiongozi huyo wa kanisa katoliki mjini Rome Desemba mwaka jana. 

Muda mfupi baada ya kukamilika misa ya Jumapili, Papa Francis mwenye umri wa miaka 84 akapelekewa katika hospitali ya Rome kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa utumbo mkubwa.