Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amerejea Vatican ikiwa ni siku 11 baada ya kufanyiwa upasuaji katika hospitali moja mjini Roma. 

Papa Francis alifanyiwa upasuaji kuondoa sehemu ya utumbo wake. 

Duru za shirika la habari la Reuters zinasema kabla kurudi Vatican, Papa Francis alisali katika kanisa la Santa Maria Maggiore. 

Papa Francis mwenye umri wa miaka 84 tangu afanyiwe upasuaji, alionekana kwa mara ya kwanza mbele ya umma Jumapili iliyopita alipozungumza kwa takriban dakika kumi hivi. 

Mnamo mwezi Septemba kiongozi huyo wa kidini anatarajiwa kuzitembelea Slovakia na Hungary.