Yawezekana Umewekeza katika elimu yako, una kila sifa ya kupata kazi fulani lakini hupati kazi hiyo, inawezekana kabisa sababu mojawapo inayokufanya usipate kazi unayoitaka ni kutokujua kuandika barua ya maombi ya kazi.
Barua ya maombi ya kazi huandikwa kwa malengo ya kuomba kazi. Kujifunza namna sahihi ya uandishi wa barua ya maombi ya kazi si kwamba utakusaidia katika kujibu maswali pekee, bali ujuzi huu utakufanya upate kazi halisi wakati utakapo hitaji kufanya hivyo.
 

Hapa nitakuelekeza mambo yote  unayotakiwa kuyafanya unapoandika barua ya maombi ya kazi. Jifunze taratibu ili baadaye uweze kuandika barua unayotaka na uweze kupata kazi

_____
==>>Muundo wa Barua ya Maombi ya Kazi

i. Anuani ya mwandishi. Yaani anuani yako wewe unayeandika barua hiyo.

ii. Tarehe.

iii. Anuani ya anayeandikiwa.

iv. Salamu.

v. Kichwa cha habari.

vi. Kiini cha barua. Hii ni roho ya barua yako, ukikosea mahali hapa, kama unajibu swali katika mtihani, utapoteza alama. Na kama unaomba kazi halisi, utaikosa. Kiini kina aya nne:

- Katika aya ya kwanza, eleza kazi unayoomba na mahali ulipoona tangazo la kazi hiyo. Ni katika sehemu hii unaweza kutaja umri wako.

- Katika aya ya pili, eleza ujuzi wako kwa ufupi. Usieleze sana. Barua hii haipaswi kuwa ndefu kupindukia.

- Aya ya tatu eleza kwa nini upewe kazi hii wewe na si mtu mwingine. Epuka kueleza shida zako binafsi ili upewe kazi. Maneno kama, ninaomba kazi hii ili niweze kumtibia mama yangu mgonjwa kitandani, hayana msaada.

- Aya ya nne eleza uko tayari kwa usahili siku gani?

vii. Mwisho wa barua. Mwisho wa barua yako uwe na:

- Neno la kufungia. Wako mtiifu. Wako katika ujenzi wa taifa n.k

- Sahihi yako.

- Jina lako

________

==>>Kupata Mifano  zaidi ya 50 ya Barua ya Maombi ya Kazi kwa Lugha ya Kiingereza, Bofya hapo chini kulingana na taaluma yako uliyosomea.

_______

1. Cover Letter Sample for Qualified Teacher 

2.Cover Letter Sample for a French Teacher 

3.Cover Letter Sample for Economist 

4.Cover Letter Sample for an Insurance Graduate

5.Cover Letter Sample for Administrative Officer  

6.Cover Letter Sample for Human Resource Manager  

7.Cover Letter Sample for Marketing Executives

8.Cover Letter Sample for a Law Graduate

9.Cover Letter Sample for Psychologist

10.Cover Letter Sample for Accounting Graduate

11.Cover Letter/Resume Sample for Computer Science

12. Cover Letter Sample for Tourism

13. Cover Letter Sample for Logistics