Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir ametangaza kuwa Sikukuu ya Eid El-Adh’haa itakuwa Julai 21, 2021, ambapo itakuwa siku ya mapumziko kitaifa.

Sponsored: Unatafuta Kazi Serikalini na Kwenye Mashirika Binafsi? Bofya Hapa

Taarifa ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) imeeleza kuwa maadhimisho ya sikukuu hiyo kitaifa yatafanyika mkoa wa Dar es Salaam ambapo swala itafanyika katika Msikiti wa Mtoro na Baraza la Eid litafanyika hapo hapo.

Mufti ametumia nafasi hiyo kuwatakia Waislam na Watanzania wote sikukuu njema na amewaomba kusherehekea kwa usalama na amani huku wakiendelea kuchukua tahadhari dhidi ya UVIKO-19.