Mahakama moja ya China umemuhuku kifungo cha miaka 18 jela tajiri katika sekta ya kilimo Sun Dawu kwa makosa kadhaa ya uhalifu uliotajwa kama uchochezi wa matatizo. 

Bilionea huyo na muungaji mkono wa harakati za kutetea haki za binadamu alihukumiwa na mahakama hiyo katika kesi iliyoendeshwa kwa siri. 

Mahakama iliyoko Gaobeidian karibu na mji wa Beijing imesema kwamba Sun alikuwa na hatia ya makosa ya uhalifu ikiwemo kukusanya watu kushambulia taasisi za kiserikali na kusababisha usumbufu wa shughuli za kiserikali na kuchochea matatizo. 

Tuhuma hizo mara kwa mara hutumiwa dhidi ya wakosoaji wa China. Bilionea huyo alikamatwa na polisi Novemba mwaka jana pamoja na jamaa zake 19 na washirika wake wa kibiashara baada a kampuni yake kuingia kwenye mvutano wa ardhi na kampuni inayomilikiwa na serikali ambayo ni mshindani wake kibiashara. Aidha mahakama pia imemtoza bilionea huyo faini ya dola 475,000 jana.