Aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump, amewasilisha kesi dhidi ya Kampuni kubwa za Teknolojia za Google, Twitter na Facebook pamoja na Watendaji Wakuu wake kutokana na marufuku aliyowekewa

Januari mwaka huu, Akaunti za Trump katika Mitandao ya Kijamii zilizuiwa kufuatia hofu ya Usalama wa Umma kutokana na ghasia zilizotokea jengo la Bunge, zikiongozwa na wafuasi wake

Trump amezilaumu Kampuni hizo pamoja na Wanademocrat ambao amewashutumu kuchochea taarifa za upotoshaji.