Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imemwachia huru Mousa Twaleb, dereva teksi aliyetuhumiwa kuhusika kumteka mfanyabiashara Mohamed Dewji. 

Twaleb ameachiwa baada ya jamhuri kusema haina nia ya kuendelea na kesi hiyo. Dewji alitekwa Oktoba 2018 kwa siku tisa.