Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametoa maagizo saba kwa watumishi wa wizara hiyo, likiwemo la kumsimamisha kazi Afisa Ugavi wa Bonde la Zone Tanganyika, Victor Kaphifa kwa kosa la kufanya udalali katika wizara hiyo na kuchafua taswira ya wizara.


Maagizo mengine aliyotoa ni pamoja na kufuatilia madeni yote ya wizara pamoja na taasisi, mamlaka za maji, kukagua madeni na madai yaliyowasilisha, hoja za CAG zipatiwe majibu, kwenda kutumia fedha za wizara kwa ajili ya kuendeleza miradi ya Maji, pamoja na kwenda kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuinua sekta ya maji, kufanya kazi na TAKUKURU kuleta mfumo wa manunuzi wa kihasibu.

Aweso amesema hayo katika Mkutano na Wakaguzi wa ndani, Maafisa Ugavi na watu wa Fedha uliofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kusikiliza changamoto wanazokutana nazo katika utendaji wao.

Aweso amesema wizara ya maji haina mashamba wala viwanja hivyo hakuna haja ya kuwa na watumishi ambao ni madalali wa wakandarasi na watoa huduma, huyu mtumishi anapaswa kusimamisha ili asiendelee kuichafua Wizara.