Jeshi la Afrika Kusini limesema leo Jumatatu linapeleka wanajeshi katika mji wa kibiashara wa Johannesburg na mkoa wa Kwa Zulu-Natal ili kukabiliana na ghasia zilizoibuka kufuatia kifungo cha rais wa zamani Jacob Zuma.
Ghasia zimeendelea kuripotiwa katika wakati mahakama inajitayarisha kusikiliza pingamizi lililowasilishwa na upande wa kiongozi huyo wa zamani dhidi ya kifungo cha jela.
Tangazo juu ya hilo linatarajiwa kutolewa baadaye.Polisi ya Afrika Kusini imesema watu 6 wameuawa na wengine 219 wamekatwa.Rais Cyril Ramaphosa amesema "Mali imeharibiwa. Magari yamepigwa mawe. Watu wametishiwa na wengine wamejeruhiwa.
Nimesikia kuwa kuna watu wamekufa. Hivi ni vitendo vinavyohatarisha maisha na vinarudisha nyuma juhudi zetu za kujenga uchumi".Mahakama ya katiba mnamo June 29, ilimhukumu Zuma kifungo cha miezi 15 jela kwa kupuuza agizo la mahakama. Rais huyo wa zamani alianza kutumikia kifungo hicho kuanzia Alhamisi wiki iliyopita.