Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, amefanya mazungumzo na viongozi wa Vatican kuhusu hatua za kuushughulikia mgogoro nchini Venezuela wakati akiwa ziarani katika makao makuu hayo ya Kanisa Katoliki duniani. 

Blinken ni afisa wa kwanza wa ngazi za juu chini ya serikali ya Rais Joe Biden kukutana na Papa Francis katika kikao kilichofanyika faragha.

Aidha Blinken alikutana pia na Kardinali Petro Parolin anayehusika na mambo ya nje ya taasisi hiyo ya kiimani, Vatican. na Askofu Mkuu Paul Gallagher anayehusika na masuala ya uhusiano wa nje wa kanisa hilo ambapo wamejadili kuanzia migogoro nchini Venezuela, Syria, Lebanon, Belarus na Ethiopia, kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani. 

Blinken amesisitiza uungaji mkono wa Marekani katika kurudisha demokrasia nchini Venezuela na nia yao ya kutaka kuwasaidia wananchi wa Venezuela kuijenga upya nchi yao. 

Pia takwenda kusini mwa Italia kushiriki mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za kundi la G20 utakaozungumzia hatua ya kuimarisha ushirikiano miongoni mwa mataifa kuhusu mabadiliko ya hatia nchi, afya na maendeleo.