Watu watano wamefariki dunia mkoani Morogoro katika ajali ya barabarani iliyohusisha magari matatu.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim amesema ajali hiyo iliyotokea katika eneo la Nanenane imehusisha basi dogo la abiria aina ya Coaster, Lori na gari ndogo ya kubeba abiria (Taxi).

Ametaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni uzembe wa dereva wa Coaster ambaye alitaka kuyapita magari yaliyopo mbele yake bila kuchukua tahadhari.

Basi hilo dogo lilikua linatoka mkoani Dar es salaam kuelekea mkoani Mbeya na Lori ambalo ni mali ya kampuni ya Dangote lilikuwa linatokea Morogoro kwenda Dar es salaam.