Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ameipongeza Serikali ya Nigeria kwa kuamua kuifungia Twitter nchini Nigeria, “Hongera sana Nigeria kwa kuifungia Twitter, Nchi nyingine ziige pia zifungie Twitter na Facebook maana zinaminya uhuru wa kujieleza”

Itakumbukwa Trump alifungiwa kutumia mitandao Twitter na Facebook January 2021 huu akidaiwa kuchochea vurugu kwenye majengo ya Bunge Marekani zilizosabisha vifo vya Watu zaidi ya wanne.

"Wao ni nani hata wawe wanaamua kipi kizuri na kipi kibaya wakati wao wenyewe ni wabaya? najilaumu kwa kutowafungia nilipokuwa Rais lakini Mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg aliendelea kunipigia simu na kuja Ikulu ya White House kwa chakula cha jioni akiniambia jinsi nilivyokua mzuri”

Wiki iliyopita Nigeria ilifungia Twitter nchini humo kwa madai kwamba shughuli za mtandao huo zinahujumu na kuingilia uhuru wa Nigeria kama Nchi huru, hatua hiyo ilichukuliwa siku kadhaa baada ya post ya Rais Muhammadu Buhari kuondolewa kwa kukiuka kanuni za mtandao wa huo wa kijamii.