Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameagiza shule zote na Taasisi za Juu za Elimu zifungwe kuanzia leo June 07,2021 kwa siku 42 kufuatia kuongezeka kwa kasi kwa maambukizi ya Corona Mashuleni.
Museveni amesema Walimu wote watapaswa kupewa chanjo kabla ya Shule na Vyuo kufunguliwa.
“Kuna ongezeko kubwa la maambukizi Mashuleni tangu March, Wagonjwa 948 wameripotiwa kwenye Shule 43 kutoka Wilaya 22 na naamini namba ni kubwa zaidi Shule nyingine hazitoi takwimu kwakuwa hawataki zifungwe na wengi wanawaza pesa tu” Museveni.